Jumatatu, 29 Agosti 2016

MKWASA AMPUMZISHA DIDA TAIFA STARS, YULE KIPA MTAMU WA JKT APATA ULAJI

Kocha Mkuu wa timu ya Mpira wa Miguu Tanzania ‘Taifa Stars’, Charles Boniface Mkwasa, amefanya mabadiliko kwenye kikosi kinachotarajiwa kusafiri Jumatano Agosti 31, 2016 kwenda Nigeria kwa ajili ya mchezo wa mwisho wa kuwania kucheza fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON 2017) dhidi ya timu ya taifa ya nchi hiyo, Super Eagles. Mabadiliko yaliyofanyika ni kwa kumchukua Kipa kinda wa JKT Ruvu, Said Kipao kuchukua nafasi ya Deogratius Munishi ambaye amefiwa na baba yake mzazi katika kifo kilichotokea jijini Dar es Salaam jana Agosti 28, 2016. Kipao alikuwa nyota wa mchezo katika mechi ya Ligi Kuu Bara dhidi ya Simba na mechi ikaisha kwa sare ya bila bao huku yeye akionyesha umahiri mkubwa wa kuokoa michomo ya washambuliaji na viungo wa Simba. Licha ya mchezo huo wa Septemba 3, 2016 kuwa sehemu ya mchuano wa kuwania nafasi ya kucheza fainali hizo za AFCON 2017 huko Gabon, lakini utakuwa ni wa kukamilisha ratiba baada ya Misri kufuzu kutoka kundi G ambalo mbali ya Nigeria na Tanzania, pia ilikuwako Chad ambayo iliyojitoa katikati ya mashindano. Wachezaji wanaounda kikosi hicho kwa sasa na kuanza kuingia kambini Hoteli ya Urban Rose jijini Dar es Salaam ni: Makipa- Said Kipao – JKT Ruvu Aishi Manula – Azam FC Mabeki Kelvin Yondani - Young Africans Vicent Andrew - Young Africans Mwinyi Haji - Young Africans Mohamed Hussein – Simba SC Shomari Kapombe - Azam FC David Mwantika - Azam FC Viungo Himid Mao - Azam FC Shiza Kichuya – Simba SC Ibrahim Jeba – Mtibwa Sugar Jonas Mkude – Simba SC Muzamiru Yassin – Simba SC Juma Mahadhi - Young Africans Farid Mussa Tenerif ya Hispania Washambuliaji Simon Msuva - Young Africans Jamal Mnyate – Simba SC Ibrahim Ajib – Simba SC John Bocco - Azam FC Mbwana Samatta - Genk ya Ubelgiji

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni