Jumamosi, 27 Agosti 2016

SPURS ITAFUTA UTEJA WA MIAKA MINNE DHIDI YA LIVERPOOL?

Siku ya Jumamosi klabu ya Liverpool itakuwa tena ugenini kwa mara ya tatu mfululizo tangu kuanza kwa msimu wa 2016/17 ligi kuu nchini England. Wataenda kwenye uwanja wa Whitehart Lane kupambana dhidi ya Tottenham Hotspurs ambayo haijapata ushindi dhidi ya Liverpool kwa miaka takribani minne. Utakuwa ni mchezo mzuri kuutazama ukizingatia zimepita mechi saba za EPL tangu Spurs ilipoifunga Liverpool 2-1 kwa mara ya mwisho November 2012. LIVERPOOL Liverpool ina udhaifu kwenye safu yake ya ulinzi, imeruhusu magoli matano ndani ya mechi mbili dhidi ya Arsenal pamoja Burnley. Pia kukosekana kwa Kiungo Emre Can ambaye alipata majeraha katikati ya wiki wakati wa mechi ya ligi kutapunguza ufanisi katika safu ya kiungo cha ulinzi. Lakini uwepo wa washambuliaji Divack Orig, Daniel Sturridge na Saido Mane ni faida kwa kocha Jurgen Klopp kuchagua nani aanze kwenye safu ya ushambuliaji. TOTTENHAM HOTSPURS Spurs haina rekodi nzuri dhidi ya Liverpool kwa miaka ya karibuni. Pia Washambuliaji wa Spurs, Harry Kane mfungaji bora wa EPL msimu uliopita pamoja na Vicent Janssen ambaye amejiunga na Spurs akitokea AZ Akmaar ya nchini Uholanzi watajaribu kufunga kwa mara ya kwanza tangu kuanza kwa msimu mpya wa 2016/17 Kocha wa Spurs, Mauricio Pochettino atalazimika kumtumia golikipa Michel Vorm kutokana na kipa namba moja Hugo Lloris kusumbuliwa na majeruhi. UTABIRI Liverpool wanajivunia historia jambo litalochangia kuingia uwanjani wakijiamini. Lakini Bado safu ya ulinzi imeonesha udhaifu katika mechi mbili za ligi. Spurs wapo imara kila idara hivyo kuna asilimia kubwa ya kufanya vizuri kwenye ambao utafanyika uwanja wao wa nyumbani. Spurs 3 – 1 Liverpool

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni