pata dondoo mbalimbali za michezo ya ndani na nje ya nchi.mompondazy itakujuza kila kitu.
Jumamosi, 27 Agosti 2016
JKT RUVU YAIPIGA STOP SIMBA
Baada ya kupata ushindi wa magoli 3-1 kwenye mchezo wake wa kwanza dhidi ya Ndanda FC, imba SC imejikuta ikibanwa na maafande wa JKT Ruvu na kulazimishwa suluhu (0-0) katika mchezo wa ligi ku Tanzania bara uliomalizika kwenye uwanja wa taifa.

Laudit Mvugo (kulia) akitafuta mbinu ya kumtoka beki wa JKT Ruvu Hassan Matelema
Simba ilipambana kutafuta goli dakika zote za mchezo lakini mambo yalikua magumu kwao kutokana na kazi nzuri iliyokuwa ikifanywa na golikipa wa JKT Ruvu Said Kipao.

Ibrahim Ajib aliingia kipindi cha pili kuchukua nafasi ya Frederick Blagnon lakini haikutosha kuisaidia Simba kupata ushindi mbele ya JKT Ruvu

Wachezaji wa Ruvu JKT wakitoka uwanjani baada ya kufanikiwa kupata pointi moja mbele ya Simba
Licha ya kufanya mabadiliko kipindi cha pili kwa kuwatoa Fedrick Blagnon na Jamal Mnyate na kuwaingiza Mwinyi Kazimoto na Ibrahim Ajib lakini bado hawakuweza kubadili matokeo.
Ikumbukwe May 21 2016, JKT Ruvu waliikomalia Simba na kuitandika bao 2-1 kwenye mchezo wao wa mwisho wa ligi kuu msimu uliopita.

Kocha wa Simba Joseph Omog akitoa maelekezo kwa wachezaji wake

mchezaji wa Simba Jamal Mnyate akijaribu kumdhibiti mchezaji wa JKT Ruvu
Matokeo hayo yanaifanya Simba kufikisha pointi 4 baada ya mechi mbili wakati JKT Ruvu wao wamefanikiwa kupata pointi 1 kwenye mchezo wao wa ufunguzi VPL msimu huu.
Vikosi vilikuwa kama ifuatavyo:
Simba: Vicent Angban, Malika Ndeule, Novalty Lufunga, Method Mwanjali, Mohamed Hussein, Jonas Mkude, Shiza Kichuya, Mzamiru Yassin, Laudit Mavugo, Fredrick Blagnon/Ibrahim Ajib, Jamal Mnyate/Mwinyi Kazimoto.
JKT Ruvu: Michael Aidan/James Msuva/Nashon Naftali, Said Kipao, Salum Gila,Nurdin Mohamed, Rahim Juma,Ismail Amour Hassan Matemela, Hassan Dilunga, Atupele Green, Saady Kipanga, Pera Mavuo.
Matokeo ya mechi nyingine zilizochezwa leo kwenye viwanja vingine:
Mtibwa Sugar 2-0 Ndanda FC
Azam FC 3-1 Majimaji FC
Tanzania Prisons 1-1 Ruvu Shootings
Mbao FC 0-1 Mwadui FC
Kagera Sugar 0-0 Stand United
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni