pata dondoo mbalimbali za michezo ya ndani na nje ya nchi.mompondazy itakujuza kila kitu.
Jumatano, 31 Agosti 2016
Nchi saba, ikiwemo wenyeji Uganda, watashiriki katika michuano ya Cecafa 2016 ya wanawake mwezi Septemba. Kenya, Burundi, Zanzibar, Ethiopia, Tanzania bara na Rwanda watashiriki. Michuano hii imethibitishwa na shirikisho la soka la Afrika Mashariki na Kati- Cecafa - mjini Kampala. Katibu mkuu wa Cecafa Nicholas Musonye amesema walitarajia kupata timu moja kutoka kusini mwa Afrika lakini hawakufanikiwa. Rais wa shirikisho la soka la Uganda Injinia Moses Magogo amesema: "Tumefurahi kuandaa michuano hii. Huu ni muendelezo wa mradi wa mkakati wa kukuza soka la wanawake nchini Uganda na katika eneo zima." Michuano hiyo itaanza Septemba 11 hadi 20 katika mji wa Jinja. Burundi na Zanzibar zitacheza katika mechi ya ufunguzi. makundi ni kama ifuatavyo. Kundi A: Uganda, Kenya, Burundi, Zanzibar Kundi B: Ethiopia, Tanzania bara, Rwanda.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni