Jumanne, 30 Agosti 2016

MBEYA CITY NAO WAMO, WAFUNGULIWA KESI RUNDO ZA KUTOLIPA MISHAHARA

Klabu ya Mbeya City, nayo imeingia kwenye listi ya kuwa moja ya klabu zinazodaiwa kutolipa mishahara wachezaji wake. Maana yake, Mbeya City ni kati ya timu zenye malimbikizo ya mishahara kama ambavyo kesi ilivyofikishwa kwenye Shirikisho la Soka Tanzania (TFF). Kamati ya Katiba, Sheria na Hadhi za Wachezaji ya TFF, iliyokaa jana imepokea kesi za Mbeya City kuhusiana na wachezaji kadhaa kudai kutolipwa mishahara yao. Them Felix, Erick Mawala na Abdallah Juma wameishtaki Mbeya City juu ya fedha za mishahara na usajili. Raymond Wawa, Simba imetia fora kwa kuwa na kesi nyingi zaidi. Coastal pia imezifungulia mashtaka Mbeya City, Kagera Sugar, JKT Ruvu juu ya fedha za fidia za wachezaji Fikirini Bakari na Ayub Yahaya (Mbeya City), Ibrahim Sheku (Kagera), Yusuf Chuma (JKT) ambao wote watamalizana ndani ya wiki moja. Them Felix, Erick Mawala na Abdallah Juma wameishtaki Mbeya City juu ya fedha za mishahara na usajili. Hii inaingiza Mbeya City kwenye doa na kuonekana haina tofauti na klabu nyingine kwa kuwa awali ilionekana ni moja ya klabu zisizokuwa na migogoro katika masuala ya mishahara. Nao, Lipuli wamefikisha malalamiko dhidi ya Mbeya City wakitaka fedha za usajili za mchezaji Mackyanda Makolo pamoja na dhidi ya JKT Ruvu wakitaka fedha ya usajili, ada ya mkoa na wilaya ya mchezaji Khasim Kisengo. Aidha, Kocha wa Serengeti Boys, Bakari Shime ameishtaki Mgambo Shooting kudai milioni 8.5 za mshahara na Mgambo wamekubali kumlipa ndani ya wiki tatu. Edward Christopher, Said Omary na Omary Seseme dhidi ya Toto African kwa madai ya fidia ya mishahara na usajili, zote ndani ya wiki moja wanatakiwa kuwa wamemalizana. Rajab Isihaka na Said Mketo wameifungulia mashtaka Ndanda wakidai mishahara na fedha za usajili, watatakiwa kumalizana ndani ya wiki hii. Akademi ya Kinondoni (Kisa) imezifungulia mashataka Azam kwa mchezaji Omary Maunda, Kagera Sugar (Hussein Abdallah), Mtibwa Sugar (Daniel Jemedari), Toto (Jafar Jafar), Majimaji (Joseph Njovu) na JKT Ruvu (Najima Maguru) ikidai fedha za malezi za wachezaji hao.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni