pata dondoo mbalimbali za michezo ya ndani na nje ya nchi.mompondazy itakujuza kila kitu.
Jumatano, 31 Agosti 2016
WARAKA WA HART WENYE HUZUNI KUBWA KWENDA KWA MASHABIKI WA MAN CITY
Joe Hart ametoa shukrani zake za dhati kwa washabiki wa Manchester City kwa sapoti yao kubwa waliyomwonesha katika kipindi cha wiki hizi chache ambazo alikuwa akipitia wakati mgumu hali iliyopelekea kutolewa kwa mkopo kwenda kunako klabu ya Torino.
Licha kuondoka Manchester City, Joe Hart bado ana mkataba na klabu hiyo mpaka mwaka 2019.
Kipa huyo ambaye alikuwa tegemeza kwa kipindi kirefu sana ameamua kuandika barua iliyojaa hisia kali na kupost kwenye ukurasa wake wa Facebook.
Ujumbe wake unasomeka hivi: “Ningependa kutumia fursa kuwaambia washabiki wote wa Manchester City nanma gani ninavyowakubali kwa mchango wenu mlioonesha kwangu.
“Kwa wiki kadhaa sasa nimepitia kipindi kigumu lakini sitaweza kusahau safari ndefu iliyojaa mafanikio ambayo nimeyapata kwenye klabu yenu hapo
“Kunzia siku ya kwanza niliposajiliwa klabuni hapo mwaka 2006, klabu na washabiki kwa ujumla walinipa faraja kubwa kwenye maisha yangu na niseme tu nawashukuru sana kwa hilo.
“Soka ni mchezo wa aina yake, na kutokana na sababu mbalimbali, sasa naondoka kwenda klabu nyingine na kufungua ukurasa mpya wa maisha yangu, na niseme tu kwamba nawashukuru sana Torino kwa kunipa fursa ya kuichezea klabu hii kubwa.
“Lakini niseme tu kwamba, hisia nilizopata hivi karibuni kwenye mchezo dhidi ya Steaua Bucharest (mchezo wake wa mwisho kabisa kuvaa jezi ya Man City wiki iliyopita) utabaki kwenye kumbukumbu zangu daima. Nawashukuru sana kwa kumbukumbu mliyoniachia.
“Kuna watu wengi mashuhuri klabuni hapo ambao hawaonekani lakini mchango wao ni mkubwa sana kwa maendeleo ya klabu, hivyo ningependa kuitakia klabu ya Manchester City, wafanyakazi wake na wachezaji na bila kusahau mashabiki wote mafanikio mema kwenye msimu huu na mingine inayofuata.”
Hart alijiunga na Manchester City mwaka 2006 na ameshinda makombe mawili ya Ligi Kuu England, Kombe la Ligi (mara mbili) na Kombe la FA.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni