Jumatano, 31 Agosti 2016

ACACIA YAVUNJA RASMI MKATABA NA STAND UNITED, WALIOIKIMBILIA KAZI KWAO

Kampuni ya uchimbaji madini ya ACACIA Gold Mine ya Bulyanhulu ya mkoani Shinyanga imevunja rasmi mkataba wa kuifadhili klabu ya Stand United. Ikumbukwekwe klabu ya Stand United ilikuwa ni klabu yenye mkataba wa udhamini uliokuwa ukiingizia mkwanja mrefu kuliko timu nyingine yeyote inayoshirikiki VPL. ACACIA imeamua kuvunja mkataba huo kwa kwa muda uliosalia baada ya mgogoro mkubwa wa kiuongozi ulioibuka kwenye klabu hiyo, ACACIA imeamua kujitoa ili kukwepa migogoro hiyo hali ambayo huenda ikasababisha mzigo mzito kwa waliochukua timu na huenda ikawa vigumu kuiendesha kama walivyotarajia. July 8, 2015, ACACIA walitia saini kuidhamini klabu ya Stand United kwa makataba wa miaka miwili unaotajwa kufikia thamani ya shilingi za Tanzania bilioni 2.4.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni