Jumatano, 31 Agosti 2016

KAKA YAKE POGBA ASAJILIWA UHOLANZI

Mathias Pogba, pacha wa Patrick na kaka wa Paul Pogba amesajiliwa na klabu ya Sparta Rotterdam ya Uholanzi kwa mkataba wa mwaka mmoja, huku kukiwa na kipengelea cha kuongeza mkataba endapo mchezaji huyo ataonesha kiwango kitakachowaridhisha mabosi wake. Kungo huyo mwenye miaka 26, ambaye amewahi kucheza kwenye timu za England kama Crawley Town, Wrexham and Crewe Alexandra amejiunga na Rotterdam baada ya mkataba wake na timu ya Partick Thistle ya Scotland kukatishwa kwa maridhiano ya pande zote mbili. “Ujio wa Mathias Pogba unatuongezea uimara kwenye safu yetu ya kiungo na ushambuliaji,” amesema Kocha Mkuu wa Rotterdam Pastoor “Ukumbwa wa umbile lake na uimara wake pia utachangia sana kuifanya timu icheze vizuri kutokana na mfumo wetu, bila ya kusahau uzoefu wake mkubwa katika mechi za kimataifa aliopata kwenye ligi za Scotland na Italy.”

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni