Jumatano, 31 Agosti 2016

OFFICIAL- STOKE CITY WAKAMILISHA USAJILI WA BONY

Stoke City wamethibitisha kumsajili kwa mkopo mshambuliaji wa Manchester City Wilfried Bony. Nyota huyo wa Ivory Coast atatumia msimu mzima kukipiga kwa Makuli hao huku kukiwa na makubaliano ya Man City kulipwa kiasi cha paundi mil 2 kutokana na huduma anayowapa. Bosi wa Stoke Mark Hughes amesema: “Ujio wa Wilfried naweza kusema siwezi kuutilia shaka yoyote, kwasababu anaijua vizuri ligi ya England na ameweza kufunga magoli mengi sana kwenye ligi hii. “Ana nguvu, kasi na ana mchango mkubwa sana linapokuja suala la matumizi ya nguvu kwenye utafutaji wa goli, bila ya kusahau ufundi wake mkubwa wa kufunga. “Miezi 18 iliyopita alisajiliwa kwa kiasi kikubwa cha fedha, hivyo tulifahamu kwamba tunapata straika wa kiwango cha juu kabisa.”

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni