pata dondoo mbalimbali za michezo ya ndani na nje ya nchi.mompondazy itakujuza kila kitu.
Jumamosi, 27 Agosti 2016
KOCHA JKT RUVU AMETAJA KILICHOWAFANYA WASHINDWE KUIFUNGA SIMBA
Baada ya pambano la ligi kuu Tanzania bara kati ya JKT Ruvu vs Simba kumalizika kwa sare ya bila kufungana, makocha wa timu zote waliuzungumzia mchezo huo uliokuwa wa kwanza kwa JKT Ruvu ambao ndio walikuwa wenyeji wakati Simba kwao ukiwa ni mchezo wa pili tangu kuanza kwa msimu mpya wa ligi 2016-17.
Kocha wa timu ya Jeshi la Kujenga Taifa Malale Hamsini amesema kushindwa kutumia nafasi kwa safu yake ya ushambuliaji ni jambo ambalo limewakosesha ushindi kwenye mchezo dhidi ya Simba.
“Tumepoteza nafasi nyingi, lakini tutalifanyia kazi hilo hasa kwa kuongeza nguvu katika nafasi ya ushambuliaji” alisema kocha huyo wa zamani wa Ndanda FC.
Kocha msaidizi wa Simba Jackson Mayanja amesema, timu yao kukosa ushindi mbele ya JKT Ruvu ni sehemu ya matokeo ya mchezo wa soka ambapo si kila mechi timu inaweza kupata matokeo inayohitaji.
“Mpira ndivyo ulivyo, kuna siku unacheza vizuri lakini hupati matokeo unayohitaji.”
Kuhusu Ajib kuanzia benchi huku raia wa Ivory Coast Frederick Blagnon akianza, Mayanja alisema: “Ni moja ya mbinu za mpira, mechi iliyopita aliingia kutokea benchi na kufunga goli, mchezo wa leo mwalimu akaamua kumuanzisha”.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni