pata dondoo mbalimbali za michezo ya ndani na nje ya nchi.mompondazy itakujuza kila kitu.
Jumatatu, 29 Agosti 2016
YANGA YATOA SHARTI ILI KWENDA KUCHEZA AZAM COMPLEX
Baada ya Azam kutoa malalamiko ya kuzuiwa kuutumia uwanja wao wa Azam Complex kucheza mechi zinazohusisha Azam FC dhidi ya vilabu vya Simba na Yanga hata kamza Azam ni mwenyeji wa michezo hiyo, Kaimu Katibu Mkuu wa Yanga SC Baraka Deusdetith amesema wao wako tayari kwenda kukipiga Chamazi endapo taratibu na mambo ya kikanuni yatazingatiwa hasa ya kiusalama.
“Kama Azam wakikubaliana na TFF wakikubaliana mchezo ukachezwe Azam Complex, makubaliano ambayo yatazingatia usalama na amani, tuko tayari kwenda kucheza. Wakati mwingine mbona tunakwenda kucheza mikoni ? Ni suala la taratibu tu, wakisema kila kitu kiko sawa sisi hatuwezi tukapinga”, amesema Deusdetith wakati alipozungumza na kipindi cha michezo cha Sports Extra.
TFF imekuwa ikiizuia klabu ya Azam FC kuutumia uwanja wa Azam Complex kwa mechi zake za nyumbani kwa madai uwanja huo ni mdogo na hauwezi kukidhi idadi ya mashabiki wa vilabu vya Simba na Yanga.
Licha ya uwanja huo kuruhusiwa na CAF kuchezewa mechi za kimataifa, bado TFF inakataa uwanja huo kutumiwa na Azam FC kwa ajili ya mechi zinazohusisha Simba na Yanga.
Ukakasi unakuja pale TFF inaposhindwa kutaja hadharani ni uwanja unatakiwa kuwa na uwezo wa kubeba idadi ya mashabiki wangapi ili uruhusiwe kutumiwa na klabu inayocheza dhidi ya Simba au Yanga.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni