Ijumaa, 26 Agosti 2016

KUNA MCHEZAJI ATAINGIA AU KUTOKA OLD TRAFFORD KABLA YA DIRISHA LA USAJILI KUFUNGWA?

Kocha Manchester United Jose Mourinho amezungumza na vyombo vya habari kuelekea mchezo wao dhidi ya Hull City. Lakini akizungumza mambo mengi bila kuipa kipaumbele Hull baada ya kuulizwa maswali kuhusu dirisha la usajili linalokaribia kufungwa hivi karibuni. Akiwa tayari amefanya usajili wake mapema baada ya kufunguliwa dirisha la usajili, Manchester United sasa inaangalia tu mambo yanavyokwenda kwenye pilika za soko la usajili. United iliwanunua Eric Bailly, Henrikh Mkhitaryan, Zlatan na Paul Pogba katika dirisha la msimu huu wa usajili na sasa Mourinho amesisitiza hakutakuwa na mchezaji atakayetoka wala kuingia.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni