Ijumaa, 26 Agosti 2016

BAADA YA TETESI ZA HART KUTUA LIVERPOOL, UKWELI UKO HIVI…

Inaonekana muda wa Joe Hart umekwisha ndani ya kikosi cha Manchester City. Golikipa huyo alipewa nafasi ya kucheza katikati ya wiki huku wengi wakiamini kuwa huo ndiyo ulikuwa mchezo wake wa mwisho mbele ya mashabiki wa nyumbani. Baada ya usajili Claudio Bravo kutoka Barcelona, Pep amedhihirisha wazi Hart siyo golikipa namba 1 wa City na ameonesha yuko tayari kumwachia Hart aondoke. Lakini sasa tatizo limekuwa ni Hart kupata klabu inayomuhitaji. Iliaminika Everton walivutiwa na golikipa huyo lakini Ronald Koeman amekanusha taarifa hizo mapema wiki hii. Hart angependa kusalia kwenye ligi ya EPL kwahiyo sasa wakala wake anatakiwa kufanya harakati za kumtafutia mahali atakapocheza. Liverpool hawajatoa offer kwa ajili ya Hart. Kwa mujib wa Echo, majogoo hao wa jiji la Liverpool hawana mpango wa kusajili golikipa licha ya kuwepo kwa tetesi zinazomhusisha Hart kuelekea Anfield. Matatizo aliyonayo golikipa wa Klopp Simon Mignolet, yangetumiwa na kocha huo kama sababu ya kumsajili Hart baada ya golikipa namba mbili Loris Karius kupata majeraha ya mkono. Lakini Echo wamesisitiza kwamba, Liverpool hawatomsajili Hart na Klopp hana mpango wa kufanya usajili wa golikipa (ana magolikipa watatu akijumuishwa na Alex Manninger).

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni