Na Athumani Adam Tetesi zimekuwa kweli mapema wiki hii pale Arsene wenger alipokamilisha usajili wa beki Shkodran Mustafi. Usajili wa beki huyo Mjerumani mwenye miaka 24 kutoka klabu ya Valencia ya kule nchini Hispania utasaidia kuziba nafasi zilizopo kwenye safu ya ulinzi ya Arsenal ukizingatia Per Mertesacker bado anasumbuliwa na majeraha Ikiwa bado mashabiki wa Arsenal wana furaha ya ujio wa Mustafi, makala hii inakupa historia fupi kabla ya kuja Arsenal. HISTORIA Shkodran Mustafi alizaliwa tarehe 17 April 1992 kule Bad Hersfeld nchini Ujerumani. Wazazi wake ni raia wa Albania wenye asili ya Marcedonia. Mwaka 2006 alijiunga na timu ya vijana ya Hamburger SV AKATAA OFA YA MAN CITY NA NEWCASTLE Mwaka 2009 klabu za Man City pamoja na Newcastle United zilitaka kumsajili Mustafi lakini akataa na kuelekea zake kule Merseyside kwenye klabu ya Everton ACHEZA. GAME MMOJA TU EVERTON Tangu ajiunge na Everton hadi anaondoka mwaka mwaka 2012, Mustafi alicheza mechi moja tu. Mechi ambayo Mustafi alicheza ilikuwa dhidi ya Bate Borisov michuano ya Europa League. Ilikuwa kwenye uwanja wa Goodson Park December 16, 2009 mchezo ambao Everton ililala 1-0 Baada ya kuona hapati nafasi ya kutosha kucheza, mustafi alimwomba kocha David Moyes kuhama Everton na kulelekea kwenye klabu ya Sampdoria. AFUNGA GOLI LAKE LA KWANZA SAMPDORIA (MECHI 53, GOLI 1) Mustafi alifunga goli lake la kwanza kama mchezaji “professional” kwenye mechi ya Serie A dhidi ya Atlanta October 2013. Sampdoria ilikuwa imepanda daraja kutoka Serie B tangu iliposhuka mwaka 2011. Mbali na Mustafi pia Samporia walikuwa na wachezaji vijana Simon Zaza na Mauro Icardi DAU LA USAJILI LAWA SIRI VALENCIA (MECHI 78, GOLI 6) Mustafi alijiunga na Valencia mwaka 2014 akitokea Sampodria bila dau la usajili kuwekwa wazi. Zipo tetesi kwamba japo haikuwekwa wazi, lakini Mustafi alitua kwa Euro milioni 8. Ndani ya Valencia Mustafi alicheza mechi 78 na kufunga goli 6. ALIKUWEPO WORLD 2014, EURO 2016 Mustafi likuwepo kwenye kikosi cha Ujerumani kilichotwaa kombe la dunia kule nchini Brazil mwaka 2014. Alipata kuitwa kwenye kikosi na kocha Joackim Low baada ya kuumia kiungo Marco Reus. Mustafi aliingia kutokea sub kwenye mechi dhidi ya Portugal na Ghana. Bahati mbaya aliuumia wakati mashindano yanaendelea Mbali na kombe la dunia pia mustafi alikuwepo kwenye mashindano ya euro 2016 kule nchini Ufaransana.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni