pata dondoo mbalimbali za michezo ya ndani na nje ya nchi.mompondazy itakujuza kila kitu.
Jumapili, 28 Agosti 2016
SIASIA AIKACHA NIGERIA
Samson Siasia aliyekiongoza kikosi cha wanaume cha Nigeria kushinda medali ya shaba kwenye michuano ya Rio Olympic amejiuzulu nafasi hiyo kwa kile alichodai kuwa ni mfumo uliokosa nidhamu kwao.
Siasia, kocha mwenye mafanikio makubwa kwenye soka la Afrika kwenye michuano ya Olympics akiwa amewahi kutwaa medali ya fedha Beijing mwaka 2008, amelalamika kwamba hajalipwa na waajari wake (Nigeria Football Federation (NFF) kwa muda wa miezi kadhaa.
Amesema ameachana na soka la Nigeria baada ya kupambana kwenye michuano ya Olympics iliyomalizika nchini Brazil.
“Nimefikia ponti ambapo naweza kusema sasa inatosha hapa nilipofikia,” Siasia ambaye mkataba wake umemalizika baada ya michuano ya Olympics aliiambia BBC Sports.
“Nimekuwa silipwi kwa miezi kadhaa, miaka mingi nimekuwa siheshimiwi na mamlaka ya soka Nigeria lakini sasa imetosha.”
“Licha ya kutwaa medali ya shaba kwenye michuano ya Olympics nchini Bralzil lakini wachezaji, makocha na maafisa wote wa timu hawajapokea pongezi zozote wala asante,” aliongeza Siasia.
Kabla ya kuwasili Brazil, kikosi cha Brazil kilizuiliwa Atlanta, Marekani kwasababu ya matatizo ya malipo ya tiketi za ndege na walitua Brazil saa chache kabla ya mechi yao ya ufunguzi waliyoshinda 5-4 dhidi ya Japan.
Nigeria pia ilijikuta kwenye matatizo kabla ya mchezo wake war obo fainali dhidi ya Denmark baada ya wachezaji kugoma kufanya mazoezi kutokana na madai ya kutolipwa kwa muda mrefu.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni