Jumanne, 30 Agosti 2016

KAMATI YA MAADILI YALITEMA SUALA LA KESSY, SASA LITAPANGIWA SIKU, SIMBA WAWASILISHA USHAHIDI

Suala la beki Hassan Kessy limechukua sura mpya baada ya kuanza kusikilizwa na Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji. Lakini imeelezwa kwamba litangiwa siku nyingine. Kamati hiyo ilikaa jana na kuwajumuisha viongozi mbalimbali wa Simba pia Yanga kwa ajili ya utetezi. Taarifa zinaeleza, Simba imewasilisha ushahidi wake ambao unaonyesha kuwa Kessy alijiunga na Yanga kabla ya mkataba wake kwisha. Suala hilo linamfanya Kessy awe amevunja mkataba na kulazimika kuangalia nini kinatakiwa baada ya kuvunja mkataba. Tayari TFF imemruhusu Kessy kuendelea kucheza wakati kamati hiyo ikiwa ndiyo imeanza kusikiliza kesi hiyo. Simba wamekuwa na uhakika kama watafanya vizuri katika kesi hiyo kwa kuwa vilelelezo kwamba alivunja mkataba kusaini mkataba mwingine na Yanga huku akiwa bado ule wao na yeye ukiwa haujaisha, uko wazi. "Kweli Simba wamewasilisha ushahidi wao na inaonekana ni kama kila kitu kipo vizuri, sasa hatujui itakuwaje, vizuri tuache suala hilo lishughulikiwe baadaye," kilieleza chanzo.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni