pata dondoo mbalimbali za michezo ya ndani na nje ya nchi.mompondazy itakujuza kila kitu.
Jumamosi, 27 Agosti 2016
MKWARA MZITO!! MADIWANI MBEYA MARUFUKU KUSAFIRI NA MBEYA CITY
Mkuu wa mkoa wa Mbeya Amos Makala amepiga marufuku Madiwani kutumia fedha za serikali kusafiri na timu Ya Mbeya City, Makala amesema hayo ni matumizi mabaya ya fedha wakati akihutubia kikao cha kusikiliza kero za wananchi ikiwa ni utaratibu aliojiwekea kila mwisho wa mwezi.
“Ule utaratibu wa Madiwani kusafiri na timu ya Mbeya City kila sehemu, kupewa posho na mafuta sasa marufuku. Ni maamuzi yasiyo na tija, kwani wao ni makocha? Wanaisaidiaje timu ya Mbeya City kupata ushindi?kibali cha kutoka nje ya mkoa anakitoa Mkuu wa mkoa.”
“Ni bora fedha hizo wapewe wachezaji kama motisha kuliko madiwani wanaozunguka na timu, nimeanza kazi.”
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni