Jumatatu, 29 Agosti 2016

GENK YAENDELEZA USHINDI UBELGIJI

Baada kufanikiwa kupata ushindi Alhamisi iliyopita na hatimaye kufuzu hatua ya makundi ya michuano ya Europa League, klabu ya KRC Genk anayoitumikia Mbwana Samatta imeendeleza matokeo ya ushindi kwenye ligi ya Ubelgiji kwa kuitandika Zulte-Waregem kwa goli 1-0. Bao pekee kwenye mchezo huo uliopigwa kwenye uwanja wa nyumbani wa Genk (Cristal Arena) limefungwa na Alejandro Pozuelo dakika ya 80. Katika mechiyo, Samatta alicheza kwa dakika 87 kabla ya kumpsha Kumordzi. Genk iko nafasi ya tatu kati ya timu 16 kwenye msimamo wa ligi imefikisha pointi 10 baada ya kucheza mechi tano

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni