Jumanne, 30 Agosti 2016

SIMBA KUMBURUZA KESSY MAHAKAMANI

Klabu ya Simba imejiridhisha na kupeleka ushahidi kwenye kamati ya sheria na hadhi za wachezaji kuhusu sakata la usajili linalomhusu beki wa kulia wa Yanga Hassan Kessy Ramadhani na wanaamini endapo haki itasimamiwa vilivyo basi watashinda kesi hiyo. “Yanga walituandikia barua, TFF wakiomba kupewa leseni ya mchezaji Kessy kabla ya June 15 ambapo ndio ulikuwa mwisho wa mkataba wake, tena walikuwa wanamuombea leseni ya CAF lakini kimantiki huwezi kupewa laseni ya CAF bila kuwa na leseni ya ndani”, amesema Haji Manara afisa habari wa Simba wakati akizungumza na waandishi wa habari. “Kwahiyo kimsingi, Kessy alivunja mkataba, Yanga walimchezesha mchezaji ambaye aliwekewa pingamizi.” Wakati huohuo klabu ya Simba imepanga kumpeleka Kessy mahakamani wakimtuhumu kuwatuhumu baadhi ya viongozi wa Simba kutaka kumpa rushwa wakati akiwa Mtibwa Sugar. “Hatutaki kuombwa radhi kwasababu katutuhumu kila mtu kasikia nchi nzima, lazima akathibitishw mahakamani. Lakini akanithibitishie mimi niliwahi kumwambia yeye atachoma banda”, alimalizia Manara.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni