pata dondoo mbalimbali za michezo ya ndani na nje ya nchi.mompondazy itakujuza kila kitu.
Jumamosi, 27 Agosti 2016
Bundesliga: Baada ya usajili mzuri, Dortmund vitani kumaliza utawala wa Bayern vs Mainz
Borussia Dortmund kwa mara nyingine tena wanategemewa kuwa wapinzani halisi wa Bayern Munich kwenye mbio za ubingwa msimu huu. Walianza msimu vyema kwa kuifunga Eintracht Trier 3-0 katika michuano ya DFB Cup wikiendi iliyopita. Shinji Kagawa alifunga mara mbili na usajili mpya Andre Schurrle alifunga lingine. 
Borussia Dortmund walikuwa active sana kwenye dirisha la usajili linalotarajiwa kufungwa siku kadhaa zijazo na timu yao inaonekana kuimarika zaidi kuliko msimu uliopita. Usajili mpya wa Ousmane Dembele kutoka Rennes, Marc Bartra kutoka Barcelona, Raphael Guerreiro kutoka Lorient, Gotze na Sebastian Rode kutoka FC Bayern na Andre Schurrle kutoka Wolfsburg. Ilkay Gundogan, Mats Hummels, Moritz Leitner na Henrikh Mkhitaryan wote waliondoka. Kiwango cha BVB kwenye pre season kilikuwa bora, walishinda mechi 3, wakapoteza mbili na sare 1.
Mainz
Mainz walikuwa na msimu mzuri mwaka jana na wakafanikiwa kumaliza nafasi ya 6 katika Bundesliga. Watacheza katika Europa League msimu huu, lakini hilo linaweza kuwadhuru kiwango chao kwenye ligi. Hawakuwa active sana kwenye soko la usajili la kiangazi na hivyo kikosi chao hakina uimara mkubwa. Hawakusajili mchezaji yoyote mkubwa, lakini wakapoteza wachezaji wawili muhimu. Mhispaniola Jose Rodriguez alijiunga na timu akitokea Galatasary, lakini wakampoteza Julian Baumgartlinger aliyehamia Bayer Leverkusen pamoja na golikipa Loris Karius aliyehamia Liverpool.
Mainz walipata matokeo mchanganyiko wa matokeo katika pre season na bado wanahangika kurudi kwenye form yao. Wiki kadhaa zilizopita walipata matokeo ya kuvutia kwa kuwafunga 4-0 Liverpool katika mchezo wa kirafiki, lakini wikiendi iliyopita walipata taabu sana kuwaondoa kwenye mashindano timu dhaifu ya Unterhaching kwa mikwaju ya penati, baada ya kumaliza muda wa kawaida kwa sare ya 3-3 katika muda wa kawaida.
Mifumo/Staili za uchezaji
Football ni mchezo wa uvumilivu na subira na haya yataonekana katika mchezo wa leo. Mainz ni timu ambayo inacheza kwa kushambulia bila kuchoka ili kuwaondoa wapinzani wao nje ya eneo lao. Pia wanapenda kukaa na mpira muda mrefu katika mechi.
Mainz watakuwa wanapeleka sana mashambulizi mbele, hivyo kuacha eneo kubwa la nyuma wazi. Dortmund wamekuwa wakifanikiwa sana kwa kucheza mchezo wa mashambulizi ya kushtukiza tangu msimu uliopita na leo watatumia mchezo huo huo kuwamaliza wapinzani wao ambao wanapenda kukabia juu kwenye eneo la uwanja.
Takwimu
*Götze alifunga 22 katika awamu yake ya kwanza na Dortmund – namba sawa ya magoli aliyoifungia Bayern Munich kwa miaka 3 aliyokaa Allianz Arena.
*Career ya kocha Schmidt inafanana na ile ya kocha wa BVB, Tuchel: Wote walianzia maisha yao ya ukocha katika klabu ya Mainz – wakitokea timu za watoto.
*Clemens Schmidt amepoteza mechi 7 kati ya 8 zilizopita dhidi ya Dortmund, ushindi pekee aliopata vs BVB ilikuwa mwaka 2014 alipokuwa kocha wa Schalke.
*Borussia Dortmund vs FSV Mainz, mchezo huu umeshachezwa mara 20 mpaka sasa. Katika michezo hiyo 20 kumekuwepo na wastani wa kufunga magoli 2.5 kwa mechi. Katika mechi 20, BVB wameshinda mechi 11, Mainz wameshinda mechi 3 na sare 6.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni