Jumapili, 28 Agosti 2016

YANGA 3-0 AFRICAN LYON 'LIVE' FULL TIME KUTOKA UWANJA WA TAIFA

Yanga 3-0 African Lyon FULL TIME! Mwamuzi anapuliza kipenga kumaliza mchezo, baada ya bao hilo, mwamuzi anaweka kati kisha mpira unamalizika. Dakika ya 90 + 4:Chupukizi aliyeingia, Yusuph anapata mpira na kuwatoka mabeki wa Lyon, anampatia Mahadhi pasi ambaye anapiga shuti kali na kujaa wavuni. GOOOOOOOOOOOOOOOO!!! Deusi Kaseke anatoka anaingia chipukizi Yusuph Mhilu. Dakika ya 90 + 2: Lyon wanaonekana kukata tamaa, Yanga wanakuwa wanacheza wao muda mwingi. Dakika ya 90: Mwamuzi wa akiba anaonyesha dakika nne za nyongeza. Dakika ya 89: Kaseke anakosa nafasi baada ya kucheza vizuri na Tambwe. Dakika ya 88: Donald Ngoma anatona na nafasi yake inachukuliwa na Matheo Anthony. Dakika ya 85: Lyon wanafanya shambulizi lakini inakuwa faulo kutokana na mshambuliaji wao kumsukuma Bossou. Dakika ya 79: Yanga bado wanaongoza mabao 2-0. Dakika ya 77: Yanga wanafanya mabadiliko, anatoka Msuva anaingia Juma Mahadhi Dakika ya 77: Lyon wanakosa nafasi ya wazi, Ramadhani Kipalamoto anabaki yeye na Dida, anapiga shuti lakini anakosa. Dakika ya 75: Lyon wanapata faulo nje ya eneo la 18 la Yanga, wanapiga lakini inakuwa offside. Dakika ya 65: Yanga wanaonekana kuelewana na kucheza ile staili yao ya 'kampa kampa tena' Dakika ya 63: Yanga wamecharuka, wanaanza kufanya mashambulizi makali, Msuva anapata nafasi nyingine anakosa. Dakika ya 60: Simon Msuva anafunga bao zuri, anapokea pasi ndefu kutoka kwa Kamusoko, Msuva anamptoka kipa wa Lyon na kutupia wavuni, Yanga mbili, Lyon hawajapata kitu. GOOOOOOOOOOO!!!!!! Dakika ya 51: Mchezo umesimama kwa muda, kuna mchezaji wa Lyon ameumia, anapata matibabu uwanjani. Dakika ya 48: Luona wanaendelea kujipanga na wameingia kwa kasi tofauti na ilivyokuwa kipindi cha kwanza, inaonekana wanataka kusawzisha bao mapema. Dakika ya 46: Kipindi cha pili kimeanza. Mwamuzi anapuliza kipenga cha kukamilisha kipindi cha kwanza, timu zinaenda kupumzika Yanga ikiongoza bao 1-0. Dakika ya 45 + 2: Hamad Tajiri anapewa kadi ya njano kwa kumchezea faulo Msuva. Dakika 45 + 2: Muda wowote kuanzia sasa mchezo utakuwa ni mapumziko. Dakika ya 45: Mwamuzi wa akiba anaonyesha zinaongezwa dakika tatu. Dakika ya 44: Yanga wanatulia na kupigiana pasi vizuri, Ngoma na Tambwe wanaonekana kuelewana. Dakika ya 43: Lyon wanafanya mashambulizi makali katika lango la Yanga, mchezaji Hood Mayanja anamtoka Bossou na kupiga shuti kali linatoka nje ya lango na kuwa goal kick. Dakika ya 40: Matokeo bado Yanga wanaongoza kwa bao 1-0 lililofungwa na Msuva. Dakika ya 38: Hali ya hewa ni ya ubaridi kiasi kwa kuwa kulikuwa na manyunyu katika baadhi ya mitaa ya Dar. Lyon nao wanamka lakini Yanga wanapiga pasi ndefu kuwa kuanzia nyuma. Dakika ya 36: Lyon wanafanya shambulizi, kipa wa Yanga, Dida anaupangua mpira huo na kisha mabeki wa Yanga wanautoa. Dakika ya 33: Yanga wanapiga faulo lakini inaokolewa. Dakika ya 32: Yanga wanapata faulo nje ya eneo la lango la African Lyon. Dakika ya 29: Yanga wanaendelea kuumiliki mpira muda mwingi wa mchezo. Dakika ya 20: Yanga wanaendelea kucheza vizuri, Lyon wamepunguza staili yao ya kucheza kwa kutegea wapinzani wao waotee 'off site trick'. Dakika ya 18: Deusi Kaseke anaipatia Yanga bao la kwanza baada ya mabeki wa Lyon kujua ameotea, kisha akamchambua kipa vizuri. GOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOO!!!! Dakika ya 10: Mchezo bado haujashika kasi sana kwa kuwa timu zote zinaonekana kucheza kwa kusomana Dakika ya 15: Yanga wanaonekana kujipanga na kufanya mashambulizi kadhaaa Dakika ya 7: Yanga wanashindwa kupata bao, Tambwe anabaki yeye na kipa lakini shuti lake linatoka nje ya lango. Dakika ya 5: Bado matokeo ni 0-0, mchezo haujawa na kasi. Dakika ya 1: Mchezo umeshaanza. Kikosi cha Yanga kilichoanza 1. Deo Munishi ‘Dida’ 2. Hassan Kessy 3. Haji Mwinyi 4. Andrew Vincent ‘Dante’ 5. Vincent Bossou 6. Thaban Kamausoko 7. Simon Msuva 8. Haruna Niyonzima 9. Donald Ngoma 10. Amiss Tambwe 11. Deus Kaseke Sub Kakolanya, Oscar, Pato Ngonyani, Mahadhi, makapu, Mateo, Yusuph Yanga Vs African Lyon kwenye Uwanja wa Taifa, leo Jumapili, mchezo wa Ligi Kuu Bara.


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni