Jumatano, 31 Agosti 2016

GENK YAITAHADHARISHA TFF JUU YA SAMATTA

Klabu ya Genk ambayo anacheza nahodha wa Tanzania Mbwana Samatta, imetoa tahadhari kwa benchi la ufundi la Taifa Stars hasa hususan upande wa madaktari juu ya Mbwana Samatta ambaye ataungana na kikosi cha Mkwasa moja kwa moja Lagos, Nigeria kwa ajili ya mchezo wa kukamilisha ratiba ya kuwania kufuzu kucheza fainali za mataifa ya Afrika nchini Gabon mwaka 2017. Afisa habari wa TFF amethibitisha tahadhari hiyo waliyopewa juu ya usalama wa Samatta katika mchezo huo. “Kauli hii imekwenda sambamba na hali ya uchezaji wa mchezaji mwenyewe, ambapo katika maelekezo wamesema wanaheshimu timu za taifa na wiki kwa ajili ya michezo ya kimataifa ya FIFA”, Alfred alikiambia kipindi cha Sports Extra cha Clouds FM. “Genk wameshauri kwamba, kabla ya Samatta ahajacheza ni vizuri akapimwa kwanza kwasababu alipewa majukumu mazito ambapo alipewa mazoezi magumu ya kuwa fit ili kuhakikisha anaisaidia timu yake kufuzu hatua ya makundi ya michuano ya Europa League. Kwahiyo walitaka kuona anapata muda wa kupumzika lakini imebidi wamwachie kwasababu anahitajika kwenye timu ya taifa.” Tanzania dhidi ya Nigeria utakuwa ni mchezo wa kukamilisha ratiba kwasababu tayari Misri walmeshafuzu kutoka katika Kundi hilo la G.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni