Jumamosi, 27 Agosti 2016

MANENO YA JULIO BAADA YA MWADUI KUPATA USHINDI WA KWANZA VPL MSIMU HUU

Baada ya kuchezea kichapo kwenye mchezo wao wa ufunguzi wa ligi mzimu huu, hatimaye Agosti 27 Mwadui FC chini ya Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ imepata ushindi wake wa kwanza kwenye mechi za ligi katika msimu mpya. Shukrani kwa Abdallah Seseme aliyeifunga goli pekee katika mchezo huo na kuipa pointi tatu za ugenini timu yake ya Mwadui kwenye uwanja wa CCM Kirumba baada ya dakika 90 kumalizika wakiwa wameichapa Mbao FC kwa bao 1-0. “Nafurahia pointi tatu lakini sijafurahia timun yangu ilivyocheza, niseme tu uwanja wa CCM Kirumba mgumu na vijana wangu hawajapata utulivu wa jinsi gani ya kucheza katika uwanja huu lakini kwasababu leo tumepata pointi tatu nashukuru” amesema Julio mara baada ya timu yake kupata ushindi wa kwanza kufatia kupoteza mchezo wao wa kwanza mbele ya Toto Africans katika uwanja huohuo. “Timu hizi ambazo zinapanda, ni timu nzuri kinachowasumbua ni uzoefu lakini wako vizuri.” Kwa upande wake kocha wa Mbao FC mrundi Etiene Nderegije amewapongeza wapinzani wake kwamba wamecheza vizuri kwasababu walipata nafasi moja na wakaitumia. “Kupoteza mechi moja haimaanishi kwamba tutapoteza matumaini, ila niwapongeze wapinzani wetu walipata nafasi moja na wakalinda goli lao.”

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni