Jumatatu, 29 Agosti 2016

VIGEZO ALIVYOVITAJA BOSS WA AZAM, SIMBA NA YANGA HAZIKWEPI KUCHEZA AZAM COMPLEX

Katika vitu ambavyo vimechukua headlines katika soka la bongo hivi karibuni ni pamoja na Azam kutaka kuutumia uwanja wao wa Azam Complex katika mechi zote ambazo wanakuwa wenyeji dhidi ya Simba na Yanga. Juma lililopita afisa habari wa Azam FC Jafar Idd alithibitisha Azam kupeleka barua TFF wakiomba kupewa haki ya kuutumia uwanja wao kwa ajili ya mechi za Simba na Yanga lakini ombi hilo liligonga mwamba kwasababu zilezile za kila siku ambazo ni udogo wa uwanja huo kubeba mashabiki wa timu hizo kongwe hapa Bongo. Sasa Agost 29, Sports Bar ya Clouds TV ilimualika Mtendaji mkuu wa Azam FC Saad Kawemba ambaye zamani alishawahi kuwa Mkurugenzi wa mashindano pale TFF. Katika vitu ambavyo aliombwa kuvitolea ufafanuzi akiwa Sports Bar ni pamoja na vigezo vinavyoupa uwanja sifa ya kutumiwa kwa ajili ya mechi za ligi pamoja na mashindano mbalimbali. “Ili uwanja uwe umekamilika lazima uwe na vigezo sita (6)”, alisema Kawemba kabla ya kuanza kuorodhesha vigezo mbalimbali vya uwanja unaokidhi mahitaji ya kitaifa na kimataifa ili kuweza kuruhusiwa kutumika kwa mechi za mashindano mbalimbali. Katika kuorodhesha vigezo ambavyo vinaufanya uwanja kupata kibali cha kutumiwa kwa mashindano, Kawemba alitaja vigezo vifuatavyo; Lazima uwanja uwe umekaguliwa na kuthibitishwa na idara husika ambapo kwa Tanzania ni lazima uwe umethibishwa na Wizara au idara ya Ujenzi kwamba uwanja unaweza kutumiwa Uwanja huo ni lazima uwe na control room kwa maana ya chumba maalum amcho ukikaa unaweza kuuona uwanja wote kupitia kamera za CCTV. Fan lights ambazo zitaruhusu mechi kuchezwa wakati wowote, si lazima iwe usiku lakini inawezekana hali ya hewa ikabadilika kukawa na mawingu au ukungu kwa hiyo taa hizo zitaruhu mechi kuchezwa bila usumbufu. Kama mechi itakuwa inarushwa moja kwa moja kupitia television taa hizo zitasaidia mtazamaji aliyeko nyumbani kupata picha nzuri. Uwanja uwe na chumba cha huduma ya kwanza na uwe na chumba cha kufanyia dopping endapo hilo litalazimika kufanyika basi huduma hiyo ipatikane. Eneo la kuchezea (pitch) vipimo vyake lazima viwe minimum, medium au maximum kulingana na vipimo vinavyotolewa na FIFA. Upatikanaji wa uwanja, uwanja lazima uwe huru pale unapotakiwa kutumika kwa ajili ya mechi. Isitokee kukawa na mechi ya ligi lakini uwanja ukawa na shughuli nyingine nje ya soka kama ilivyotokea CCM Kirumba, Mwanza lilipofanyika tamasha la Fiesta mechi ikaahirishwa. Asilimia 80 ya watu wataoingia uwanjani wawe wamekaa, hapa kanuni haitaji asilimia 80 ya mashabiki wangapi bali ni asilimia ya 80 ya mashabiki waliopo uwanjani. Kuwe na uzio unaowatenganisha wachezaji na mashabiki kwasababu sehemu salama wakati mpira unachezwa ni kwenye pitch. Baada ya hayo yote, swali kwa TFF ni je, kwanini viwanja kama Manungu Complex unaotumiwa na Mtibwa Sugar na ule wa Mabatini unaotumiwa na Ruvu Shootings vimeruhusiwa kutumiwa kwenye mechi za VPL vikiwa havina viti vya mashabiki na havitambuliwi hata na CAF lakini Azam Complex unaotambuliwa na CAF Simba na Yanga zisiende kucheza?

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni