Jumanne, 30 Agosti 2016

OFFICIAL- ARSENAL WAMEMSAJILI PEREZ KUTOKA DEPORTIVO LA CORUNA

Arsenal wamekamilisha usajili wa mshambulizi wao mpya Lucas Perez kutoka klabu ya Deportivo La Coruna. Meneja wa Arsenal Arsene Wenger Jumamosi alithibitisha kwamba Perez (27) pamoja na beki kutoka Valencia Shkodran Mustafi walikuwa wamefikia maridhiano binafsi, huku akiahidi kuwatabulisha leo. Hata hivyo, Washika Bunduki hao hawafafanua ni kiasi gani hasa wametumia kumsajili na wamempa mkataba wa muda gani licha ya kuarifiwa kwamba amenunuliwa kwa ada ya paundi mil 17. “Huyu si tu mfungaji, bali ni mchezaji ambaye anaweza kuleta muunganiko mzuri na wenzake, anaweza pia kupiga pasi za mwisho bila kusahau uwezo wake mkubwa wa kujitenegenezea nafasi za kufunga,” Wenger ameiambia tovuti ya klabu hiyo. “Ana jicho la goli na alikuwa na kwenye kiwango bora msimu uliopita.” Kabla ya kujiunga na Arsenal, Perez amewahi kucheza kunako klabu za Rayo Vallecano, Karpaty Lviv, PAOK na Deportivo. Nyota huyo ambaye anasifika kwa kwa uwezo wake mkubwa uwanjani pamoja na kasi, msimu uliopita alifunga mabao 17 kwenye michezo ya ligi 36 na kutoa assists 10.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni