Jumanne, 30 Agosti 2016

HAZARD AMFANANISHA KANTE NA PANYA

Eden Hazard amemfananisha kiungo mpya wa Chelsea N’Golo Kante na panya kutokana na uwezo wake mkubwa wa kuzunguka uwanja mzima pindi awapo uwanjani . Nyota huyo wa Ubelgiji amevutiwa sana na aina ya uchezaji wa Kante kutokana na matumizi yake makubwa ya akili na nguvu panapohitajika. Kante, ambaye ni raia wa Ufaransa msimu uliopita alishinda kombe la EPL akiwa na Leicester City kabla ya kuhamia Darajani msimu huu. Hazard aliimabia Chelsea TV: ‘Anatupa uwezo mkubwa wa kujiamini. Mara nyingi huwa tunajaribu kupiga chenga na kuwapita wapinzani, lakini huwa tunafanya hivyo tukiamini kwamba hata tukipoteza mpira kuna mtu yupo nyuma yetu kwaajili ya kutulinda. ‘Ni mchezaji wa aina yake. Ni kama panya vile, anazunguka uwanja mzima na ana fikra za upambanaji sana, kwa ufupi ni mchezaji wa kiwango cha juu kabisa. ‘Mara nyingi ni faraja sana kucheza na wachezaji wa kiwango cha juu.’


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni