Alhamisi, 25 Agosti 2016

MESSI ASHINDA TUZO YA GOLI BORA LA UEFA

Kabla ya kuanza kwa hatua ya makundi ya michuano ya klabu bingwa Ulaya, mtandao wa UEFA.com umemtangaza Messi kuwa ameshinda tuzo ya goli bora la michuano hiyo msimu uliopita. Goli lililompa Messi tuzo hiyo ni lile alilofunga wakati Barcelona ikicheza dhidi ya AS Roma kwenye msimu uliopita (2015-16). Messi alifunga goli hilo kwa ku-chop mpira kwa ustadi akimalizia pasi kadhaa za haraka-haraka zilizopigwa eneo la hatari la Roma kabla ya kufunga goli hilo. Nyota huyo wa Barcelona ameshinda tuzo hiyo baada ya kupata 34% ya kura zote.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni