Alhamisi, 25 Agosti 2016

SAMATTA AENDELEA KUING'ARISHA GENK, ATUPIA BAO MCHUJO WA EUROPA TIMU YAKE IKISHINDA 2-0

Mbwana Samatta ambaye ni nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania, amefunga bao na kuisaidia KRC Genk ya Ubeligiji kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Lokomotiva ya Zagreb. Bao la Samatta lilikuwa mapema kabisa katika dakika ya kwanza ya mechi hiyo ya mchujo kuwania kucheza Europa.  Bao la pili, pia lilifungwa mapema katika kipindi cha pili na pacha wa Samatta, Leon Bailey. Samatta ameonekana kuwa msaada mkubwa katika upachikaji mabao katika kikosi cha Genk.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni