pata dondoo mbalimbali za michezo ya ndani na nje ya nchi.mompondazy itakujuza kila kitu.
Jumatano, 24 Agosti 2016
MUGABE AAGIZA POLISI KUWAKAMATA WANAMICHEZO WALIOCHEMSHA OLYMPIC BRAZIL
Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe amemwagiza mkuu wa Polisi wan chi hiyo Augustine Chihuri kuwakamata wachezaji wote wa timu iliyokwenda inchini Brazil kwenye mashindano ya Olympic mara tu watakapokanyaga kwenye ardhi ya uwanja wa ndege wa Harare.
Zimbabwe ni miongoni mwa mataifa ambayo wanamichezo wake hawakufanikiwa kushinda medali ikiwa inawakilishwa na wanamichezo 31. Mchezaji ambaye alionekana kufanya vizuri ni yule aliyekamata nafasi ya nane
Mugabe amemwambia mkuu huyo wa polisi kuwakamata wanamichezo hao: Tumepoteza pesa za taifa kwa ajili ya hao panya tunaowaita wanamichezo. Kama hauko tayari kujitoa na kushinda japo medali ya shaba kama wenzetu wa Botswana walivyofanya, sasa kwanini ulienda kupoteza pesa zetu” alisema.
Kama tulihitaji watu kwenda Brazil kuimba wimbo wetu wa taifa na kupeperusha bendera, tungewaagiza warembo na vijana watanashati kutoka Chuo Kikuu cha Zimbabwe wakatuwakilishe.
Akaongeza kwamba, pesa iliyowekezwa kwenye timu ili kuiwakilisha inchi ingeweza kutumiwa kununulia dawa na kujenga shule. Jambo hili ni sawa na mwanaume asiyelijali kuoa wanawake watano, maana yake nini? Nitahakikisha tunagawana hasara, wote watailipa serikali bila kujali hata kama itachukua miaka 10, sasa pesa hizo zinabadilika na kuwa mkopo tuliowapa kwenda Brazil kama watalii, hawana faida” akamaliza.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni