Jumatano, 24 Agosti 2016

ALICHOKISEMA JULIO BADA YA KICHAPO CHA TOTO AFRICANS

Baada ya Mwadui FC kupoteza mchezo wake wa kwanza kwenye ligi kuu Tanzania bara kwa kichapo kutoka kwa Toto Africans, kocha wa kikosi cha wachimba madini ya Almasi Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ amesema licha ya kufungwa goli kutokana na uzembe wao, mwamuzi wa mchezo huo pia hakuwa fair kwa dakika zote za mchezo. “Wanachezesha kwa kufuata watu, nafikiri hawa wajumbe wa kamati ya utendaji wanaokuwa wasimamizi wa vituo ndiyo sababu ya kufanya hivi, siwezi kumtaja mhusika. Toto wakija nyumbani nashinda, hapa tunafungwa lakini dawa bado sijaipata. Leo tumefungwa kwa uzembe wetu lakini baadaye mwamuzi hakuwa fair na mimi desturi yangu sipendi kuwasema waamuzi lakini kwakweli hawakuwa vizuri” alisema Julio baada ya timu yake kudondosha pointi tatu mbele ya Toto Africans. Mwadui wamechezea kichapo cha goli 1-0 ugenini kwenye uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza, goli lililofungwa na Waziri Junior dakika ya 34 kipindi cha kwanza bao lililodumu kwa dakika zote zilizosalia.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni