Alhamisi, 25 Agosti 2016

DEAL DONE- BRAVO ADONDOKA MINNE MAN CITY, AKAMILISHA SAFARI YA JOE HART

Manchester City wamekamilisha usajili wa Claudio Bravo kutoka FC Barcelona kwa ada ya paundi mil 17. Bravo atakuwa akijikusanyia kitita cha paundi 100,000 kwa wiki baada ya kusaini mkataba wa miaka minne aliosaini klabuni hapo, pesa ambayo ni takriban mara mbili na ile aliyokuwa akilipwa Barcelona. Barvo (33) anaweza kucheza kwa mara ya kwanza kabisa kwenye mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya West Ham utakaochezwa Jumapili jioni. Vile vile ataongezwa kwenye kikosi kitakachoshiriki Michuano ya UEFA Champions League Alishinda La Liga kwa kipindi ambacho alikuwa akiichezea Barca, japokuwa hakuvaa medali ya Uefa wakati Barca waliposhinda Champions League mwaka 2015 kwasababu hakupata nafasi ya kucheza kwenye michuano hiyo.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni