Ijumaa, 26 Agosti 2016

UEFA YAFANYA MABADILIKO CHAMPIONS LEAGUE

Shirikisho la soka la Ulaya UEFA limetangaza mabadiliko katika michuano ya UEFA Champions League kuanzia msimu ujao 2017-18. Kuanzia msimu ujao, timu 4 za juu kutoka katika ligi 4 bora barani Ulaya (La Liga, Premier League, Budesilga na Serie A) zitakuwa zinafuzu moja kwa moja kuingia hatua ya makundi bila kupitia hatua ya mtoano. Awali timu zilizoshika nafasi ya nne katika msimamo wa ligi hizo zilikuwa zinacheza mchezo wa mtoano (play off) na mshindi ndiyo anafuzu hatua ya makundi kama ilivyofanyika pia katika msimu huu.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni