Ijumaa, 26 Agosti 2016

KICHUYA ATAMANI MABAO KAMA YALE YA AMISSI TAMBWE

Kiungo mshambuliaji wa Simba, Shiza Kichuya, ametamba kuwa msimu huu atafunga mabao mengi na ikiwezekana anaweza kumpokonya tuzo ya ufungaji bora wa Ligi Kuu Bara, Mrundi wa Yanga, Amissi Tambwe. Msimu uliopita, Tambwe alichukua tuzo hiyo baada ya kufunga mabao 21 ikiwa ni mara yake ya pili kuchukua tuzo hiyo, mara yake ya kwanza ilikuwa msimu wa 2013/14 akiwa Simba ambapo alifunga mabao 19. “Mimi nina kasi na uwezo wa kufunga na kwa sasa naona kama vyote hivyo vimeongezeka, hata ukiniangalia mazoezini utagundua hilo ninalokwambia, naamini naweza kuwa mfungaji bora,” alisema Kichuya ambaye tayari ana bao moja katika ligi hiyo. Kichuya amejiunga na Simba msimu huu akitokea Mtibwa Sugar ya Turiani mkoani Morogoro. Tokea ametua Simba, ameonyesha uwezo mzuri na kuwa sehemu ya utengenezaji mabao pamoja na kuwa sehemu ya wafungaji.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni