Jumapili, 25 Desemba 2016

SIMBA UTAWAELEZA NINI KWA KIFAA CHAO HIKI KIPYA KUTOKA STAND UNITED! Mshambuliaji mpya wa Simba, Pastory Athanas ndiye mchezaji gumzo zaidi kwa kipindi hiki miongoni mwa mashabiki wa Simba. Athanas amejiunga na Simba akitokea Stand United na amekuwa gumzo baada ya kucheza mechi yake ya kwanza kwa dakika 90. Ameichezea Samba dakika 90 ikiwa ni siku chache tokea ajiunge nayo kwenye dirisha dog akitokea Stand. Katika mechi hiyo ya kwanza, ameonyesha uwezo mkubwa ikiwa ni pamoja na kuwapa wakati mgumu mashabiki wa JKT. Simba ilishinda kwa bao 1-0 na kuendelea kujishindilia kileleni huku Pastory akiwa mchezaji aliyesumbua zaidi ya wengine. Katika mchezo huo, Athanas aliongoza kwa kufanyiwa madhambi na mabeki wa JKT baada ya kumkwatua zaidi ya mara saba. Katika vijiwe mbalimbali vya soka, mitandaoni pia, Athanas ndiye anayezungumzwa zaidi.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni