Alhamisi, 22 Desemba 2016

MAN CITY YATENGA PAUNI MILIONI 50 KUMNASA BEKI WA KATI WA SOUTHAMPTON Kikosi cha Manchester City ina mpango wa kumwaga pauni milioni 50 kumnasa beki wa kati wa Southampton. Beki Virgil van Dijk ndiye anayeitoa jasho Man City ambayo chini ya Kocha Pep Guardiola inaona safe yake ya ulinzi haijatulia zaidi. Van Dijk, 25, amekuwa beki gumzo tokea kuanza kwa Ligi Kuu England msimu huh na amekuwa akionekana kufuatiliwa na timu kadhaa lakini Man City wamekuwa wa kwanza.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni