Ijumaa, 23 Desemba 2016

Hawa ni wachezaji wanaolipwa pesa nyingi duniani sasa hivi,Oscar namba 1. Baada ya kuweka wazi kwamba yeye ni mchezaji wa Shanghai SIPG hatimaye Oscar amekuwa mchezaji namba moja kwa kulipwa pesa nyingi duniani. Kwenye listi ya mishahara mikubwa Oscar anategemewa kulipwa kiasi cha pound laki 4 kwa wiki ambapo juu kidogo zaidi ya Cristiano Ronaldo ambaye analipwa kiasi cha pound 365,000. Uhamisho wa Oscar unatarajiwa kukamilija mwezi January kwenye dirisha dogo. Kwenye list hii ndani ya top 10 kuna wachezaji watatu ambao wanacheza ligi ya China ambayo inaongoza kwa kulipa mishahara mikubwa duniani. Yupo mchezaji Hulk ambae analipwa pound 317,000 kwa wiki na Graziano Pelle ambaye analipwa 260,000 kwa wiki. Hadi sasa hivi inategemewa kwamba Tevez ndiye anatawajiwa kuwa mchezaji atakayekuwa analipwa pesa nyingi zaidi kama akikamilisha uhamisho wake.Teves anatawajia kujiunga na ligi ya China na mshahara wake unatajwa kamba utakuwa Pound 600,000 kwa wiki. Tayari Teves ameshawaaga mashabiki kwenye mechi na muda wowote anatarajiwa kuiongoza listi hii kwa kuwa mchezaji anayelipwa mshahara mkubwa zaidi.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni