Alhamisi, 22 Desemba 2016

BAADA YA KUSOTA NA MATIBABU, KOTEI SASA KUMBE MAMBO FRESH TU... Hali ya kiungo James Kotei wa Simba, sasa iko vizuri kwa kuwa aligongwa na kupasuka mdomo na si kuumia hadi kwenye meno. Kotei ameanza mazoezi na anajisikia vizuri baada ya kupata usimamizi mzuri wa matibabu kutoka kwa daktari Yassini Gembe. Kotei aligongwa na kuchanwa mdomo na beki Paul Ngalema wa Ndanda FC ikiwa ndiyo mechi ya kwanza ya kiungo huyo kuichezea Simba. Ingawa Simba ilishinda kwa mabao 2-0, lakini Kotei alilazimika kwenda nje na nafasi yake kuchukuliwa na Muzamiru Yassin baada ya kuwa ameumizwa na Ngalema, jambo ambalo yeye alilaani na kusema lilitekelezwa kwa makusudi kabisa.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni