pata dondoo mbalimbali za michezo ya ndani na nje ya nchi.mompondazy itakujuza kila kitu.
Alhamisi, 22 Desemba 2016
Ngoma ‘out’ Yanga vs African Lyon Yanga itaingia uwanjani kucheza dhidi ya Yanga ikiwa bila mshambuliaji wake hatari raia wa Zimbabwe Donald Ngoma anayetumikia kadi tatu za njano. Kocha msaidizi wa Yanga Juma Mwambusi amethibitisha kuwa, kikosi chao kitacheza mchezo huo wa mzunguko wa 17 bila huduma ya Ngoma. “Bahati mbaya tutamkosa Ngoma kwasababu anakadi tatu za njano lakini pia ana majeruhi, Matheo Anthony na Beno Kakolanya pia hawa hawatahusika kabisa kwenye mchezo dhidi ya African Lyon,” anasema Mwambusi. “Wengine wote wako vizuri na watawawakilisha wenzao.” “Tumefanya mazoezi ya mwisho leo asubuhi kujiandaa na mchezo wetu dhidi ya African Lyon, ni mechi ngumu na raundi ya pili kila timu inataka kufanya vizuri ndiyo maana utaona African Lyon inaweza kutoka sare na Azam.” Ijumaa December 23 Yanga itacheza na African Lyon kwenye uwanja wa Uhuru ikiwa ni mwendelezo wa ligi kuu Tanzania bara. Yanga inakumbukumbu ya ushindi wa magoli 3-0 dhidi ya JKT Ruvu katika mchezo uliopita wakati African Lyon ilifanikiwa kuibana Azam FC na kupata suluhu.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni