pata dondoo mbalimbali za michezo ya ndani na nje ya nchi.mompondazy itakujuza kila kitu.
Jumanne, 20 Desemba 2016
MKATABA MPYA, LUKAKU KUWA ANAYELIPWA ZAIDI EVERTON Mshambuliaji Romelu Lukaku anatarajia mkataba mpya na klabu yake ya Everton ambao atakuwa akilipwa pauni 100,000. Kwa kiwango hicho cha malipo, maana yake Lukaku raia wa Ubelgiji ataweka rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza wa Everton kulipwa kiasi hicho kwa wiki. Everton ambayo nyumbani kwake ni Goodison Park jijini Liverpool, haijawahi kutoa pauni 100,000 kwa mchezaji yoyote. Lukaku alijiunga na Everton Juni, 2019 akitokea Chelsea na imeelezwa wakala wake Mino Raiola amekuwa katika mazungumzo mazito na uongozi wa Everton. Katika majira ya joto, nusura Lukaku arejee Chelsea lakini suala hilo lilishindikana baada ya mwekezaji mpya wa Everton, Farhad Moshiri kusisitiza anataka abaki
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni