pata dondoo mbalimbali za michezo ya ndani na nje ya nchi.mompondazy itakujuza kila kitu.
Jumanne, 20 Desemba 2016
KWA SIMBA SASA, BADALA YA KICHUYA, GUMZO ZAIDI NI MO IBRAHIM Mshambuliaji Mohamed Ibrahim wa Simba, ndiye amechukua nafasi kubwa ya gumzo kwa mashabiki wa klabu hiyo. Ibrahim maarufu kama Mo, ndiye mchezaji anayezungumzwa zaidi mitandaoni pamoja na mijadala ya kawaida. Gumzo la Mo, linachukua nafasi ya Shiza Kichuya ambaye alitamba katika mzunguko wa kwanza katika kikosi cha Simba. Lakini, tokea Simba imecheza mechi na kuishinda Ndanda FC, Mo anaonekana kuwa gumzo kwa kuwa ndiye alifunga bao la pili. Pamoja na kufunga bao hilo, Mo alionekana kuwa tishio zaidi kwa mabeki wa Ndanda kutokana na kuwatoka mara kwa mara na kutoa pasi kwa wenzake. Kiungo huo amejiunga na Simba akitokea Mtibwa Sugar na kadiri siku zinavyosonga mbele amekuwa akizidi kujenga imani ya kupata nafasi ya kuanza katika kikosi cha Kocha Joseph Omog. Kabla alikuwa akiingia kipindi cha pili na kila alipopata nafasi hiyo, alitoa pasi ya bao au kufunga mwenyewe. Baada ya hapo, Omog alionekana kumuamini na kumpa nafasi ya kuanza katika kikosi chake, nafasi ambayo anaonekana kuitumia vizuri.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni