Jumanne, 27 Desemba 2016

HALF SCORPION YA MKHITARYAN YAWA GUMZO, WAKO WANASEMA HATARI, WENGINE OFFSIDE Bao alilofunga kiungo Henrikh Mkhitaryan wa Manchester United ndiyo limekuwa gumzo usiku wote wa kuamkia leo. Mkhitaryan alifunga bao hilo wakati Man United ikiitwanga Sunderland kwa mabao 3-1, jana. Bao hilo lililopewa nina la “Half Scorpion”, alilifunga kwa kupiga kutumia unyayo wake wakati ikionekana kama mpira umempira. Wanaojadili wamekuwa wakijadili mambo mawili. Wako wanaosema ni offside na wengine wamekuwa wakizungumzia ubora wake na kumpongeza Mkhitaryan ambaye asili yake ni Armenia.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni