Jumanne, 20 Desemba 2016

MKATA UMEME WA YANGA MAMBO SAFI, APATA KIBALI CHA KUFANYA KAZI NCHINI Uongozi wa Yanga umefanikiwa kumaliza suala la kibali cha mchezaji Justice Zulu maarufu kama Mkata Umeme. Zulu ambaye ni kiungo mkabaji raia wa Zambia, alishindwa kuanza kuitumikia Yanga katika mechi dhidi ya JKT Ruvu baada ya kuondolewa kwenye listi na kutupwa jukwaani. Lakini taarifa za ndani kutoka Yanga zinaeleza, klabu hiyo imefanikiwa kupata kibali cha kufanya kazi na sasa atakuwa tayari kuitumikia klabu hiyo. Zulu amejiunga na Yanga akitokea Zesco ambayo ilikuwa ikinolewa na Kocha George Lwandamina.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni