pata dondoo mbalimbali za michezo ya ndani na nje ya nchi.mompondazy itakujuza kila kitu.
Jumapili, 25 Desemba 2016
MPIRA RAHA SANA, DIEGO COSTA AMEMISI PURUKUSHANI ZA PEPE, RAMOSI Mshambuliaji nyota wa Chelsea, Diego Costa amesema amewakumbuka mabeki wawili wa Real Madrid, Pepe na Sergio Ramos. Costa akiwa Atletico Madrid alikuwa msumbufu na mara kadhaa alipambana na Pepe na Ramos wakati timu hizo za jiji la Madrid zilipokutana. Ameiambia Sports Mail kwamba wachezaji hao walikuwa wakimpa changamoto ya kutosha na anawakumbuka. “Kila mmoja alijua utakuwa mchezaji wa ushindani wa juu tunapokutana. Walikuwa wababe, walicheza kwa nguvu, mimi pia nilifanya hivyo. “Kitu kizuri hakuna aliyesahau ubinadamu, mambo yote yalienda ndani ya mchezo na baada ya hapo, ilikuwa ni kawaida. Nakumbuka sana hiyo hali,” alisema. Costa sasa ni kinara wa mabao Chelsea na England na timu yake ipo kileleni mwa Ligi Kuu England.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni