Jumatano, 28 Desemba 2016

LIVE KUTOKA UWANJA WA UHURU: YANGA 3-0 NDANDA (MAPUMZIKO) MAPUMZIKO DAKIKA 3 ZA NYONGEZA Dk 45, Yanga wanafanya shambulizi jingine, safari hii Ngoma anapiga shuti, wanaokoa. Mwamuzi anasema ni offsise Dk 44, Yanga wanafanya shambulizi kali, Msuva anaingia vziuri lakini Ndanda wanaokoa SUB Dk 40 Ndanda wanamtoa Salvatory Ntebe na kumuingiza Ayoub Shabaan Dk 39, Kipa Ndanda Jeremiah anafanya kazi ya ziada kuokoa mpira wa krosi kichwani mwa Tambwe Dk 34, shuti kali la mpira wa adhabu la Kiggi, linadakwa kwa ulaiiniiii na Dida Dk 32, Yanga wanagongeana vizuri tena, Mwinyi anampa Martin pembeni, anapiga krosi lakini mabeki Ndanda wanaokoa. Dk 30 sasa, kipa wa Ndanda alikuwa anatibiwa kwa dakika mbili. Ameamka pale, mpira unarejea mchezoni KADI Dk 26, Tambwe analambwa kadi kwa ushangiliaji wake usiokuwa wa kiungwana, aliruka na kukanyaga kibendera kikavunjika GOOOOOOOO Dk 25, pasi safi, Tambwe anatulia na kuandika bao safi kabisa Dk 24, Yanga wanagngena vizuri, Niyonzima anawachambua mabeki wa Ndanda na kuachia shuti kali, lakini kipa anadaka kama nyani GOOOOOOOOO Dk 21, Ngoma anaandika bao la 37 kwa Yanga msimu, la pili kwake leo baada ya kuunganisha krosi safi kabisa kutoka kwa Juma Abdul ambayo ilimparaza beki wa Ndanda na kumfikia yeye aliyeupiga mpira na kutinga wavuni Dk 19 sasa, Yanga inaendelea kupambana vizuri na mambo yanaonekana si mazuri kwa Ndanda Dk 15, Ndanda wanapata kona yao ya kwanza, inachongwa na Ngalema, hatari hapa lakini Yanga wanaokoa Dk 13, martin wa Yanga anaingia vizuri, anajaribu kupiga shuti lakini kipa wa Ndanda anaonyesha umahiri hapa Dk 13, Kiggi Makasi anapiga mpira wa faulo, shuti kali kabisa hapa lakini Dida anadaka vizuri Dk 9 sasa, kwa hali ilivyo, Ndanda wanalazimika kubadilika, la sivyo watafungwa tena, maana wanaachia upenyo kwa Yanga kupenya mara nyingi kwenye lango lao huku wao wakishindwa kabisa kumiliki mpira muda mrefu Dk 8, Martin anawachambua mabeki wawili wa Yanga, anapiga krosi safi kabisa. Kidogooo, Tambwe anachelewa Dk 5, Juma Abdul anaachia mkwaju mkali kabisa hapa, goal kick GOOOOOO Dk 4, Ngoma anaiandikia Yanga bao saafi kwa kichwa baada ya kuunganisha mpira wa kona Dk 1, mechi inaanza kwa kasi kubwa ikionekana Yanga wamepania kupata bao la mapema.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni