pata dondoo mbalimbali za michezo ya ndani na nje ya nchi.mompondazy itakujuza kila kitu.
Jumatano, 21 Desemba 2016
Sanchez asema jiji la London lina stress sana. Alexis Sanchez amesema kwamba jiji la London lina stress sana akiwa kwenye wakati ambao kauli yake inaleta utata sana. Mchezaji huyu muhimu sana kwa club ya Arsenal yupo kwenye wakati wa kuamua future yake na club hiyo ya Arsenal kama ataendelea au atasepa. Kwa habari zilizopo sasa hivi ni kwamba Sanchez na timu yake imetaka pesa zaidi na kiasi chenyewe kinatajwa kuwa kati ya pound laki mbili na nusu hadi tatu. Sanchez akiongea na magazine moja aliulizwa kuhusu jiji la London Sanchez alisema,“Kuna wakati najaribu kutembea kwenye jiji hili nikipata nafasi lakini mara nyingi bora nibaki nyumbani tu. London kuna stress sana kwasababu kuna watu wengi sana na ni jiji kubwa”. Mara ya mwisho Sanxhez kuzungumzia kuhusu kama atasaini mkataba na Arsenal Sanchez alisema kwamba inategemea na club kama watamuamini aendelee kubaki hapo.Upande wake hakuna tatizo lolote kabisa. Kumuamini alikua anamaanisha kwamba pamoja na kutimiza matakwa yake kimaslahi. Mara nyingi mastaa wa soka huwa wanazingatia mambo mengi kabla hawajaamia kwenye club yoyote. Moja wapo ni mahali pa kuishi. Kupenda jiji flani lenye mazingira anayoyapenda nalo huchangia kwa kiasi kikubwa kwa mchezaji kukaa hapo.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni