pata dondoo mbalimbali za michezo ya ndani na nje ya nchi.mompondazy itakujuza kila kitu.
Jumamosi, 24 Desemba 2016
LIVE KUTOKA UWANJA WA UHURU: SIMBA 1 VS 0 JKT (FULL TIMEI). MPIRA UMEKWISHAAAAAA -Kichuya anaachia mkwaju hatari hapa lakini kipa anadaka vizuri DAKIKA 3 ZA NYONGEZA Dk 89 sasa, zaidi mpira unachezwa katikati ya uwanja na Simba wakiwa wameongeza ulinzi zai Dk 85, Athanas anawatoka mabeki wawili wa JKT, anamimina krosi nzuri lakini kipa yuko makini, anauhifadhi mpira mikononi mwake KADI Dk 84, Mkude analambwa kadi ya njano kwa kumuangusha Hassan matelema Dk 81, Hassan anapiga kichwa ndani ya msitu wa mabeki wa Simba, lakini ni rahisi kwa Agyei SUB Dk 80 Kassim Kisengo anaingia kuchukua nafasi ya Juma upande wa JKT SUB Dk 79, Kotei anakwenda kwenye benchi na nafasi yake anachukua Said Ndemla. Dk 78 sasa, kinachoonekana kama vile Simba wameridhika na bao hilo moja an kasi yao imepungua ambalo si jambo zuri kwao. JKT wanaonekana wana nia ya kusawazisha Dk 75, kichuya anawahadaa mabeki wa JKT, anasogea na kupiga shuti lakini kipa anadaka vizuri kabisa Dk 73, Bado mashambulizi ya JKT yanaonekana kuwa si makali ingawa kwenye mipira ya adhabu wamekuwa wakijitahidi kuamsha kashkash. Simba wamekuwa na mashambulizi mengi zaidi lakini hawako makini katika umaliziaji Dk 70, JKT wanaliandama lango la Simba na kupata kona inachongwa hapa, Mkude anautoa, kona tena. Inachongwa goal kick Dk 69, Kipa JKT anafanya kazi nyingine nzuri hapa, Kichuya anaingia na kumimina krosi safi lakini shuti la Muzamiru linadakwa vizuri na kipa huyo Dk 68, Simba wanapoteza nafasi nyingine nzuri kabisa, Kotei akiwa ameruka peke yake, anapiga kichwa lakini anashindwa kulenga lango. Goal kick Dk 67, Simba wanaukatiza msitu wa walinzi, lakini JKT wanakuwa makini zaidi kuokoa Dk 66, Muzamiru, Athanas wanagongeana vizuri kabisa. Mpira unamkuta Kichuya akiwa na kipa tu, anapiga juuuuuuu SUB Dk 62, Mo Ibrahim anakwenda benchi na nafasi yake inachukuliwa na Jamal Simba Mnyate SUB Dk 60, Atupele Green anaingia kuchukua nafasi ya Salim Gilla aliyeumia KADI Dk 59, mwamuzi anamlamba kadi ya njano Kelvin Nashon kwa kumuangusha Muzamiru Dk 58, Athanas anaingia na kuachia kombora, kipa JKT anadaka, unamtoka lakini anauwahi na kuudaka tena Dk 57, Simba wanagongeana vizuri lakini Kichuya badala ya kupiga krosi, anajaribu kufunga mwenyewe, goal kick Dk 55, Agyei anaruka juu na kuokoa mpira wa juu uliokuwa unaelekezwa langoni mwake SUB Dk 55, Ally Billa anaenda nje, Najim Magulu anaingia upande wa JKT Dk 51, Mo Ibrahim anaingia vizuri kabisa, anapiga shuti lakini mpira unakatika na kuwa goal kick SUB Dk 49, Simba wanamtoa Bukungu na nafasi yake inachukuliwa na Hamad Juma Dk 46, mpira umeenza kwa kasi lakini inaonekana kama bado kuna hali ya jazba hivi miongoni mwa wachezaji -MAPUMZIKO -Wachezaji wa JKT wanaonekana kumzonga mwamuzi hapa wakilalamika kwamba kipa wao alikuwa chini -Kipa bado yuko chini anatibiwa na mwamuzi akiwa anasubiri, anainuka hapa GOOOOOOOOO DK 45+2, Muzamiru anaifungia Simba bao akiunganisha krosi ya Athanas, wakati huo kila Seif alikuwa chini baada ya kugongwa, hakuinuka DAKIKA 3 ZA NYONGEZA Dk 44, Kipa Hamisi Seif wa JKT, mwenyewe anakwenda hadi chini na kukaa. Sasa anatibiwa Dk 43, Simba wamefanya shambulizi mfululizo kwa dakika moja nzima lakini JKT wamekuwa makini kuokoa, kipa wao wao Hamisi Seif anakuwa makini zaidi Dk 38, Simba wanahamia kwenye lango la JKT, wanafanya mashambulizi matatu mfululizo lakini JKT wanaonekana wako makini kuokoa DK 36, JKT wanafanya shambulizi jingine kali lakini shuti la Juma halikulenga lango Dk 33, krosi safi inamkuta Kichuya, anajaribu shuti baiskeli lakini mpira unatoka nje Dk 32, JKT wanapata kona baada aya kufanya shambulizi la kushitukiza, inachongwa na Mussa Juma, mpira unamkuta Mkude anaokoa Dk 29, kipa wa JKT yuko chini baada ya kuumizwa, anapatiwa matibabu huku Simba wakisubiri kupiga kona Dk 27, Simba wanapata kona ni baada ya kuendelea kupeleka presha kubwa kwenye lango la JKT Dk 23, kipa Hamisi Seif anaokoa kwa ukaribu shuti la Muzamiru baada ya krosi safi ya Pastory Dk 22 sasa, JKT wanabaki nyuma kwa wingi, wakiacha mtu mmoja tu na wanafanya mashambulizi ya kushitukiza Dk 21, JKT wanafanya kazi ya ziada kuwazuia Simba baada ya kugongeana vizuri wakiingia kwenye lango lao KADI Dk 20 Kotei naye analambwa kadi ya njano kwa kufanya madhambi KADI Dk 19 Edward Joseph analambwa kadi ya njano kwa kubaki na mpira baada ya filimbi Dk 17, Athanas anaingia vizuri hapa na kupiga shuti, beki wa Yanga anazuia na kipa anadaka vizuri KADI Dk 15, Salim Aziz Gilla analambwa kadi ya njano kwa kumuangusha Athanas Dk 11, Joseph wa JKT anaonyesha uwezo mkubwa kwa kuachia shuti kali lakini kipa Agyei anaonyesha umahiri kwa kuokoa na kuwa kona, isiyo na matunda Dk 7, Pastory anajaribu vizuri hapa akiunganisha pasi ya Kichuya lakini shuti lake halikulenga lango Dk 5 sasa, Simba wanaendelea kupanga mashambulizi lakini bado mpira zaidi unachezwa katikati ya uwanja Dk 2, Banda anapiga vizuri hapa mpira wa adhabu, lakini kipa JKT anaonyesha umakini mkubwa Dk 1, Pastory alikuwa anaondoka lakini anaangusha na kuwa faulo Dk 1, mechi inaanza kwa kasi ikionyesha kila timu imepania kupata bao la mapema, JKT ndiyo wanaanza mpira na Simba wanafanya madhambi
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni