Alhamisi, 22 Desemba 2016

SIMBA YAKAMILISHA SUALA LA VIBALI VYA KAZI VYA MAKOCHA, WACHEZAJI WAKE Uongozi wa klabu ya Simba umefanikiwa kukamilisha suala la vibali vya wachezaji na makocha wake. Serikali ilitoa agizo jana kwamba kwa wachezaji na makocha wa kigeni, hawataruhusiwa kufanya kazi hadi kila kitu kuhusiana na vibali vya kufanya kazi nchini vitakapokamilika. Lakini Simba, imefanikiwa kukamilisha zoezi hilo na wachezaji na makocha wake wa kigeni wako huru kuendelea na kazi. “Kweli kila kitu kimekamilika, wote watakuwa mazoezini,” kilieleza chanzo kutoka ndani ya Simba. Simba ina makocha wa kigeni watatu ambao ni Kocha Mkuu, Joseph Omog (Cameroon), Kocha Msaidizi, Jackson Mayanja (Uganda), Kocha wa Makipa Iddi Salim (Kenya) na wachezaji saba wa kigeni.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni