pata dondoo mbalimbali za michezo ya ndani na nje ya nchi.mompondazy itakujuza kila kitu.
Jumatano, 28 Desemba 2016
BREAKING NEWS; AZAM FC YAFANYA MIPANGO YA KUMREJESHA KALI ONGALA Saa chache baada ya Azam FC kumtimua Kocha Mkuu, Zeben Hernandez, kuna taarifa imeanza mazungumzo na Kalimangonga Ongala. Taarifa zinaeleza, Azam FC imeanza mipango ya kumrejesha Ongala aliyewahi kuwa kocha wake msaidizi kipindi cha kocha mkuu, Stewart John Hall. Kwa sasa Ongala ambaye ni mshambuliaji wa zamani wa Abajalo ya Sinza na Yanga, anainoa Majimaji ya Songea Habari kutoka ndani ya Azam FC zimeeleza, uongozi unafanya juhudi ili Kali aanze kazi wakati wa michuano ya Mapinduzi lakini kila kitu kimekuwa kikifanyika kwa siri kubwa sana. "Ni kweli hilo suala lipo, lakini uongozi unataka kulifanya kwa siri sana. Maana kuna Kali lakini bado kuna uwezekano wa kocha mwingine. Lakini uongozi unaona kocha aliye ndani hapa ndiye itakuwa poa zaidi maana anayajua mazingira," kilielea chanzo. Ongala ambaye ni mtoto wa mwanamuziki wa zamani nchini, Remmy Ongala, alikulia kisoka katika klabu ya Abajalo FC ya Sinza.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni