Jumanne, 27 Desemba 2016

Habari njema kuhusu Farid Musa. Baada ya kukwama kwa muda mrefu, hatimaye kijana Farid Musa anaondoka kwenda Spain kujiunga na klabu yake mpya ya Tenerife inayoshiriki ligi daraja la kwanza nchini Hispania (Segunda División) kwa ajili ya kucheza soka la kulipwa. Afisa habari wa Azam FC Jafar Idd amethibisha safari ya Farid Musa kwa kuonesha tiketi iliyotumwa na timu ya Tenerife ambayo ndio ataitumikia kwa mkopo. “Kama mtakumbuka tuliwaambia Farid Musa taratibu zake zinakwenda vizuri, aliitwa ubalozini akapeleka passport yake na mkataba wake na Azam FC. Ninapoongea na ninyi ni kwamba, klabu ya Tenerife ya Spain imetuma tiketi ya ya Farid Musa ambapo anatarajiwa kuondoka tarehe 28 (kesho) kuelekea Spain kujiunga na klabu yake,” anasema Jafar Idd wakati akizungumza na waandishi wa habari. Farid anataraji kuondoka kesho December 28 saa 5 usiku kwa ndege ya KLM kutoka Dar hadi Amsterdam ambapo ataunganisha hadi Barcelona kisha Tenerife. Mjadala wa Farid ulikuwa mkubwa baada ya mchezaji huyo kuchelewa kuondoka kwenda kujiunga na timu yake mpya baada ya dili lake la kusajiliwa kwa mkopo kukamilika. Nyota huyo wa timu ya taifa amekuwa nje ya uwanja kwa muda mrefu hadi nahodha wa timu ya taifa Mbwana Samatta aliwahi kuhoji.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni