Jumatano, 28 Desemba 2016

LIVE KUTOKA UWANJA WA UHURU: YANGA 4-0 NDANDA (FULL TIME) MPIRA UMEKWISHA DAKIKA 3 ZA NYONGEZA Dk 90, Ndanda wanafanya shambulizi kali hapa, Dida anaokoa GOOOOOOO Dk 88, Bossou anaiandikia Yanga bao la nne, likiwa ni bao la 39 la Yanga msimu huu katika Ligi Kuu Bara na la pili kwake msimu huu. Aliungainisha mpira wa kona Dk 87, Yanga wanapata koa yao ya sita leo baada ya NGalema kuiwahi krosi ya MSuva. Ila Ngalema yuko chini pale Dk 86, Yanga wanaendelea kutawala huku Ndanda wakiwa hawana matumaini hata ya kupata bao moja tu Dk 83, Jeremiah, kipa wa Ndanda FC anaonyesha umahiri mkubwa kuokoa mpira wa kichwa wa Msuva akiunganisha krosi Dk 80, Ndanda wanaingia vizuri, Kiggi anapiga krosi safi, kona. Hii ni kona ya pili ya Ndanda katika mechi hii, inachongwa na Mtama hapa, hakuna kitu SUB Dk 78, Yanga wanamtoa Emmanuel Martin na nafasi yake inachukuliwa na Deus Kaseke Dk 73, Omary Mponda anaachia mkwaju mkali kabisa hapa wa adhabu lakini Dida anadaka vizuri kabisa SUB Dk 70, Thabani Kamusoko anaingia kuchukua nafasi ya Haruna Niyonzima Dk 68, Yanga inaendelea kutawala mpira kwa asilimia kubwa Dk 62, Yondani anaondoa mpira ndani ya eneo la 12 la lango lake lakini yeye na Rifat Hamisi wanaanguka. Wote wawili wanatibiwa hapa SUB Dk 60 Yanga wanamtoa Said Juma 'Makapu' na nafasi yake inachukuliwa na Justice Zulu maarufu kama Mkata Umeme Dk 55 sasa, inavyoonekana, Ndanda hawana shambulizi lolote kali langoni mwa Yanga. SUB Dk 53, Abuu Ubwa anakwenda nje na nafasi yake inachukuliwa na Salum Mineli Dk 52, krosi nyingine safi ya Msuva, lakini Tambwe anajichanganya mwenyewe mpira ukiwa mguuni Dk 51, krosi safi ya Niyonzima, anapiga krosi safi, Tambwe anapiga lakini mpira unatoka nje Dk 49, Yanga wanapata kona, inachongwa vizuri kabisa hapa. Ngoma akiwa katika nafasi nzuri anapiga kichwa juuu Dk 47, krosi safi ya Juma, Tambwe anaunganisha kichwa, Ndanda wanaokoa, mpira unakuta Martin anaachia shuti kali kabisa hapa, goal kick Dk 46, mpira unaana na Yanga wanaonekana bado kuwa na uchu... MAPUMZIKO DAKIKA 3 ZA NYONGEZA Dk 45, Yanga wanafanya shambulizi jingine, safari hii Ngoma anapiga shuti, wanaokoa. Mwamuzi anasema ni offsise Dk 44, Yanga wanafanya shambulizi kali, Msuva anaingia vziuri lakini Ndanda wanaokoa SUB Dk 40 Ndanda wanamtoa Salvatory Ntebe na kumuingiza Ayoub Shabaan Dk 39, Kipa Ndanda Jeremiah anafanya kazi ya ziada kuokoa mpira wa krosi kichwani mwa Tambwe Dk 34, shuti kali la mpira wa adhabu la Kiggi, linadakwa kwa ulaiiniiii na Dida Dk 32, Yanga wanagongeana vizuri tena, Mwinyi anampa Martin pembeni, anapiga krosi lakini mabeki Ndanda wanaokoa. Dk 30 sasa, kipa wa Ndanda alikuwa anatibiwa kwa dakika mbili. Ameamka pale, mpira unarejea mchezoni KADI Dk 26, Tambwe analambwa kadi kwa ushangiliaji wake usiokuwa wa kiungwana, aliruka na kukanyaga kibendera kikavunjika GOOOOOOOO Dk 25, pasi safi, Tambwe anatulia na kuandika bao safi kabisa Dk 24, Yanga wanagngena vizuri, Niyonzima anawachambua mabeki wa Ndanda na kuachia shuti kali, lakini kipa anadaka kama nyani GOOOOOOOOO Dk 21, Ngoma anaandika bao la 37 kwa Yanga msimu, la pili kwake leo baada ya kuunganisha krosi safi kabisa kutoka kwa Juma Abdul ambayo ilimparaza beki wa Ndanda na kumfikia yeye aliyeupiga mpira na kutinga wavuni Dk 19 sasa, Yanga inaendelea kupambana vizuri na mambo yanaonekana si mazuri kwa Ndanda Dk 15, Ndanda wanapata kona yao ya kwanza, inachongwa na Ngalema, hatari hapa lakini Yanga wanaokoa Dk 13, martin wa Yanga anaingia vizuri, anajaribu kupiga shuti lakini kipa wa Ndanda anaonyesha umahiri hapa Dk 13, Kiggi Makasi anapiga mpira wa faulo, shuti kali kabisa hapa lakini Dida anadaka vizuri Dk 9 sasa, kwa hali ilivyo, Ndanda wanalazimika kubadilika, la sivyo watafungwa tena, maana wanaachia upenyo kwa Yanga kupenya mara nyingi kwenye lango lao huku wao wakishindwa kabisa kumiliki mpira muda mrefu Dk 8, Martin anawachambua mabeki wawili wa Yanga, anapiga krosi safi kabisa. Kidogooo, Tambwe anachelewa Dk 5, Juma Abdul anaachia mkwaju mkali kabisa hapa, goal kick GOOOOOO Dk 4, Ngoma anaiandikia Yanga bao saafi kwa kichwa baada ya kuunganisha mpira wa kona Dk 1, mechi inaanza kwa kasi kubwa ikionekana Yanga wamepania kupata bao la mapema.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni